Mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri amepongeza Rais Uhuru Kenyatta Kwa hotuba yake ya maridhiano na amani wakati wa maombi Nakuru.
Ngunjiri, katika mahojiano na mwanahabari huyu siku ya Jumamosi alisema kuwa hotuba ya Rais ni ya busara haswa wakati huu ambapo maridhiano ndiyo muhimu.
"Mimi nikiwa kiongozi wa Nakuru nampongeza Rais Kwa hotuba hiyo ambapo alisisitiza umoja, amani na maridhiano," alisema Ngunjiri.
Wakati huo huo, mbunge huyo wa Bahati alitoa wito kwa viongozi kuheshimiana na kujali maslahi ya wananchi.
Alisema kuwa wakati huu si wa siasa za matusi bali za kuwaunganisha wananchi kwa mustakabali wa taifa.