Siku moja tu baada ya ripoti mpya kuonyesha kuwa Kenya imeshamiri ufisadi, Mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri anasema kuwa tume ya EACC inafaa kupewa nguvu zaidi. 

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Ngunjiri anasema kuwa vita dhidi ya ufisadi vitafaulu tu iwapo tume ya maadili na kupambana na ufisadi itapewa nguvu zaidi. 

"Sharti EACC ipewe nguvu katika kushughulikia kesi za ufisadi humu nchini," alisema Ngunjiri. 

Mbunge huyo wa Bahati anasema kuwa ni jambo la kusikitisha kwamba ufisadi unazidi kushamiri humu nchini. 

Wakati huo huo, ametoa wito kwa wakenya pia kuwa macho na kuripoti visa vyovyote vya ufisadi.

Picha: Mbunge Kimani Ngunjiri wa Bahati. Ametoa wito kwa serikali kuipa nguvu EACC kukabiliana na ufisadi. PMambili/Hivisasa.com