Mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri ameitaka serikali kukabiliana vikali na wanasiasa wa mrengo wa Cord akisema kuwa wameikosea heshima huku wakivunja sheria.

Share news tips with us here at Hivisasa

Ngunjiri alidai wanasiasa wa Cord wamekuwa wakivunja sharia na kuingiza siasa katika maswala ya kisheria.

“Wanasiasa wa Cord wasifikirie wako juu ya sharia. Ni lazima watii na kuheshimu sharia kama wakenya wengine,” Ngunjiri alisema.

Hayo yanajiri wakati ambapo gavana Joho anakabiliwa na serikali baada ya kudai kuwa hatarudisha bunduki yake kama alivyodaiwa.

Joho aliagizwa na afisa wa kutoa leseni za bunduki Samuel Kimaru arudishe bunduki zake tatu.

Hata hivyo, Joho alisema hayuko radhi kurudisha bunduki hizo.