Mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri amewahimiza wakazi wa eneo bunge hilo kuendelea kujisajili kupokea vitambulisho vya kitaifa kwa wingi kwa matayarisho ya uchaguzi wa 2017.
Akiongea katika kituo cha kibiashara cha Maili Kumi na Engoshura, Ngunjiri aliwaambia wakazi kuwa ni muhimu sana kupata vitambulisho kwa wale ambao hawajasajiliwa.
"Kila mmoja wenu ajisajili kupata kitambulisho kabla zoezi hili. Kutapa kitambulisho sasa ni rahisi," alisema Ngunjiri.
Serikali kupitia wizara ya maswala ya ndani ilizindua mpango wa kupeana vitambulisho katika wadi zote nchini ili kuhakikisha wananchi wote walio na umri wa miaka 18 wamepata vitambulisho.
Shughuli hio pia inanuia kuwapa vitambulisho vya kisasa wananchi walio na vitambulisho vya kitambo.