Gavana wa Mombasa Hassan Joho amesema kuwa hana wasiwasi na usalama wake uko shwari licha ya kupokonywa walinzi wote.
Joho alisema siku ya Jumapili katika eneo la Majengo kwenye uzinduzi wa barabara, ambapo alisisitiaza kuwa yuko huru na salama hata bila walinzi kwani anajiamini kuwa hana ubaya na wananchi wake, hivyo basi hawawezi kumvamia.
Aliongeza kuwa yuko salama kutembea bila ulinzi wowote kama raia wa kawaida.
Siku kadha zilizopita, idara ya polisi iliwaondoa maafisa wake wa usalama ambao wamekuwa wakimlinda katika hali isiyoeleweka.
Maafisa hao wapatao saba kutoka idara ya polisi wamekuwa wakimpa gavana huyo ulinzi akiwa kazini na pia nyumbani kwake.