Mwaniaji wa kiti cha uwakilishi wa wanawake Kaunti ya Mombasa Bi Zamzam Mohammed akiwahutubia wakaazi katika hafla ya awali. Picha/ thecoastcounties.com
Mwaniaji wa kiti cha uwakilishi wa wanawake Kaunti ya Mombasa Bi Zamzam Mohammed amesema kuwa yuko tayari kushiriki kwenye kura za mchujo ifikapo uchaguzi mkuu.
Akiongea mjini Mombasa Bi Zamzam alisema kuwa hataogopa kamwe kushiriki kura hizo kwani wananchi ndio watakao toa uamuzi.Zamzam alishikilia kwamba ana amani ya kushinda uchaguzi huo, na kuongeza kuwa uongozi bora sio kuoneshana ubabe na mivutano ya kisiasa, bali ni kushirikiana vyema.Mwanasiasa huyo alisema yuko tayari kushirikiana na mpinzani wake endapo atashindwa kwenye mchujo.Aidha, aliongeza kuwa ni sharti viongozi wa chama cha Wiper kuhakikisha kura za mchujo zinafanyika kwa njia ya huru na haki bila kuegemea umaarufu wa mtu.Vile vile, amewasihi viongozi wanao wanaia nyadhifa mbali mbali za uongozi katika kaunti hiyo kutoogopa kushiriki kwenye kura za mchujo kwani ndio njia pekee ya kupata mfumo bora wa uongozi.Hata hivyo, amewahimiza wakaazi wa Mombasa kutotumiwa vibaya na viongozi wa kisiasa ifikapo uchaguzi mkuu na badala yake kuwachagua viongozi watakao leta mabadiliko na maendeleo.