Wanao azma ya kuwania kiti cha ubunge cha Nyaribari Chache wameombwa kushirikiana na kumuunga mkono mbunge aliye ofisini kwa sasa ili kuimarisha viwango vya maendeleo katika eneo bunge hilo.
Akiongea katika hafla ya kuchangisha pesa ugani Nyanturago soli ua Jimamosi kwa kusaidia ujenzi wa makanisa sita katika eneo bunge la Nyaribari chache wadi ya Ibeno, Mbunge Richard Tong’i alisema yuko tayari kushirikiana na wapinzani wake kisiasa ili kuleta maendeleo katika eneo hilo.
“Kwa kuleta maendeleo ni lazima tushirikiane na kuhakikisha kuwa mwanaichi wa kawaida anafaidika,” alisema Tong’i
Hafla hiyo ilionyesha ushirikiano mwema wakati makanisa ya Kiadventista na ya kikatholiki yalijumuika pamoja, huku viongozi wa kanisa mbalimbali wakiwaomba wanasiasa kufutilia mbali uhasama wao wa kisiasa ili kuleta maendeleo .
Baadhi ya waliohudhuria hafla hiyo ni Zaar Jhanda na Birundu, ambao wana azma ya kuwania kiti cha ubunge Nyaribari chache katika uchaguzi ujao.