Mwanamume mmoja ameiambia mahakama kuwa alitekeleza wizi wa mbuzi ili kugharamia matibabu ya mkewe, aliyejifungua mapacha.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Ali Goshi, anadaiwa kuiba mbuzi wa Juma Salim, mwenye thamani ya shilingi elfu saba, katika eneo la Changamwe, mnamo Juni 25, 2016.

Akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Francis Kyiambia siku ya Ijumaa, Goshi alisema kuwa umaskini na ukosefu wa ajira ndio chanzo cha kumfanya kutekeleza wizi huo.

“Hali ya uchumi na gharama za maisha ndio chanzo cha kunifanya nimuibe mbuzi huyo,” alisema Goshi.

Hatahivyo, Goshi aliiomba mahakama msamaha na kusisitiza kutorudia kosa hilo tena.

“Naomba msamaha na sitorudia kosa kama hilo tena,” alisema Goshi.

Mahakama itatoa hukumu yake mnamo Septemba 15, 2016.