Serikali ya jimbo la Nakuru itatumia takriban Sh55 millioni katika jitihada za kuwainua walemavu katika jimbo hilo, hii ni kwa mujibu wa gavana wa Jimbo hilo Kinuthia Mbugua.
Mbugua alisema kuwa fedha hizo zitakuwa zikiongezwa kila mwaka ili kuwawezesha walio na ulemavu kujiimarisha kiuchumi.
"Hatua hii itasaidia kuimarisha uchumi wa jimbo hili," akasema Mbugua.
Gavana Mbugu aliongeza kuwa kaunti hiyo haitabagua walemavu wakati inapoajiri.
Alikuwa akiongea katika hafla moja katika Shree Jalaram ambapo kirasmi alipeana vifaa vya kuwasaidia walemavu kutembea ikiwemo magurudumu na magongo ambayo ni muhimu kwa walemavu.
“Serikali yangu itawapa kipau mbele walemavu na kuhakikisha kuwa mandhari ya mahali wanafanyia biashara zao iko sawa,” akasema Mbugua.