Gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae amesema atahakikisha ameimarisha zaidi sekta ya afya katika kaunti hiyo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kulingana naye sekta hiyo ndio ya muhimu zaidi katika maisha ya binadamu haswa wanapougua na kusema atajaribu kila awezalo kuona kuwa huduma ambazo hutolewa katika hospitali mbalimbali ni za manufaa kwa wakaazi wa kaunti hiyo .

Akizungumza siku ya Jumatano mjini Kisii wakati alipokuwa anazindua magari mengine kumi ya ambulensi Ongwae alisema aliongeza magari hayo kuwa 10 katika kaunti hiyo ambayo yatafanya kazi ya kusafirisha wagonjwa ili kupata huduma za matibabu katika hospitali za kaunti hiyo kwa muda unaofaa.

“Niliona kuwa wakati tulikuwa na magari tano pekee wagonjwa walikuwa wanapata shida kusafirishwa na kufikishwa hospitalini nikaona heri serikali yangu iongeze magari mengine ambayo nimezinduia leo ili kufanya kazi ya usafirishaji,” alisema Ongwae.

Sasa kaunti ya Kisii ina magari 10 ya ambulensi huku kila eneo bunge la kaunti hiyo likipata gari moja na gari lingine litatumika katika hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Kisii.