Mbunge wa Nyali Hezron Awiti amesema kuwa atahakikisha wakaazi wa Mombasa wamepata kiongozi bora kwa kuwatetea na kupigania haki zao, ili kuhakikisha kuwa maswala muhimu ya uongozi na maendeeleo yanafanikishwa.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza mjini Mombasa siku ya Jumapili, Awiti alisema kuwa ni wakati wa viongozi wa Mombasa kuhakikisha kuwa wanapigania haki za wakaazi sambamba na kuwafanyia maendeleo, huku akiwahimiza vijana kujitokeza na kumuunga mkono.

Awiti alisema kuwa mwananchi ndiye atakayeamua nani atamchagua wakati wa uchaguzi mkuu ujao na akawahiza vijana kuwa tayari kujiunga na siasa kwani demkrasia ya nchini imeweka wazi kila jambo, huku akiwataka vijana kuungana na kufanya maendeleo mashinani.

Wakati huo huo, aliwasuta viongozi wenzake wanaowania nyadhfa mbalimbali za kisiasa kwa kusema kuwa kampeni za amani ndizo zenye msingi katika taifa hili na kuwataka viongozi hao kukoma kufanya kampeni za ukabila, chuki na uchochezi.

“Ninaomba viongozi wenzangu kufanya kampeni zao kwa njia ya amani na uiano ili kuwaunganisha Wakenya pamoja. Wale wasiopenda wenzao nawaambia kamwe hawatanitikisa,” alisema Awiti.

Kwa sasa mchakato wa kisiasa katika Kaunti ya Mombasa unaendelea kupamba moto huku viongozi mbalimbali wakionekana kujitokeza kuwania nyadhfa mbali mbali za uongozi.