Kijana wa miaka 22 na mpeziwe mwenye  umri wa miaka 17, walifumaniwa Jumatano  asubuhi na maafisa wa utawala wa mkoa wakijiandaa kutekeleza shughuli za kuavya mimba katika kata ya Ndungiri Kirima kaunti ndogo ya Nakuru Kaskazini.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akidhibitisha kisa hicho chifu mkuu wa kata hiyo Tony Kurui alidokeza kwamba alipokea habari kuhusu mpango huo, ambapo yeye pamoja na maafisa wengine wa polisi walielekea hadi nyumba walikokuwa wakiishi wawili hao ambapo walitibua njama hiyo.

Chifu huyo alisema: "Msichina huyo bado hajatueleza anasomea shule gani au hayuko shuleni, lakini amekubali kwamba anashawishiwa na mpeziwe kutekeleza unyama huo."

Kwa sasa wawili hao wamezuiliwa katika kituo cha polisi cha Bahati eneo la Maili Kumi huku uchunguzi kuhusu mpango huo haramu ikiendelezwa.

Hata hivyo chifu huyo ametoa onyo kali kwa vijana na wasichana ambao wanalenga kutekeleza tabia hiyo huku akisema watapatana na mkono wa sheria.