Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mkuu wa Idara ya Ardhi katika Kaunti ya Mombasa amesema kuwa huenda kukazuka mzozo katika Shamba la Waitiki, lililoko Likoni, baada ya masoroveya kukosa kuweka mipaka baina ya nyumba za wakazi wa sehemu hiyo.

Akihutubia wanahabari siku ya Alhamisi, Antony Njaramba aliwalaumu masaroveya waliopima shamba hilo kwa kusema kuwa ukosefu wa mipaka huenda ukaleta changamoto kubwa miongoni mwa wamiliki wa vipande vya ardhi hiyo, jambo alilolitaja kuzuwa hofu kwa wakaazi wa shamba hiyo.

Aidha, Njaramba alidokeza kuwa serikali ya kaunti ilitoa vifaa vyote vilivyohitajika katika upimaji wa ardhi hiyo, lakini wahusika wakuu wa upimaji huo tayari wamefunga zoezi hilo kwa ardhi hio ya ekari 985 na makazi 11,900.

“Iwapo tatizo hilo halitatuliwa kwa wakati unaofaa, huenda likaleta shida katika siku za usoni,” alisema Njaramba.