Mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri amemuuliza gavana Mbugua kuchukua hatua ya dharura dhidi ya bodi ya uwajiri kazi ya Nakuru.
"Namuuliza gavana kuchukua hatua mara moja dhidi ya bodi hii na wafanya kazi yake," alisema Ngunjiri.
Hayo yamejiri baada ya kubainika kwamba bodi hio imekua ikijihusisha na ufisadi ili kuwaajiri wafanyikazi wa kaunti.
Mjadala wa bunge la kaunti Jumanne uliidhinisha kupigwa kalamu kwa wasimamizi wa kaunti zote ndogo 11 na wadogo wao wakitaja kuwa waliajiriwa kinyume na sheria. Aidha ilibainika kwamba kumekuwa na uwepo wa wafanyikazi ghushi wa kaunti waliopokea mshahara kinyume na sheria.
Ngunjiri aliyasema haya kwenye ujumbe kwa wanahabari.