Waziri wa usalama wa ndani, Joseph Nkaissery ameelezea kuwa serikali ina nia ya kuwarejesha makwao wakimbizi.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Nkaissery alitoa wasiwasi wa kiusalama na ushauri wa kusafiri dhidi ya Kenya kama baadhi ya sababu za kufungwa kwa kambi. Alisema hayo wakati alkuwa anahutubia vyombo vya habari Jumatano mchana.

"Kenya inakabiliwa na matokeo mabaya kama vile ushauri kusafiri kwa makambi ya wakimbizi yanakuwa vituo vya magendo, biashara ya binadamu na kuingiza silaha kinyume cha sheria," alisema Nkaissery.

Kwa mujibu wa Nkaissery, Somalia sasa ni nchi ya amani na wakimbizi wanaweza kurudi kwao. Alibainisha zaidi kuwa Kenya haitakuwa nchi ya kwanza kufanya hivyo kwani Ulaya pia inawarejesha wakimbizi wa Syria.

Nkaissery alisema kuwa Kenya imekuwa mwenyeji wakimbizi sasa kwa miaka ishirini na tano licha ya kwamba kambi za wakimbizi wanatakiwa kuwa muda mfupi na si ya kudumu. Aliongezea kuwa damu kumwagwa na Amisom kuikomboa Somalia siyo bure.

Mchakato wa kuwarejesha wakimbizi makwao ilianza Novemba na unatarajiwa kumalizka mwishoni mwa mwaka huu.