Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho huenda akatiwa nguvuni wakati wowote baada ya kukaidi kurejesha bunduki yake aliyoagozi na idara ya usalama kufanya hivyo mara moja.
Waziri wa maswala ya ndani nchini Meja Jenerali mstaafu Joseph Nkaissery amesema gavana Joho anaweza tu kukata rufaa kuhusiana na uamuzi huo ikiwa kwanza atarejesha bunduki alizopewa na serikali kutumia kama ulinzi wake.
Kwenye taarifa yake kwa vyomb vya habari, Nkaissery amesema kuwa Joho amekuwa akionekana mwenye hasira na hali yake inaweza kumfanya atumie bunduki yake visvyo.
Nkaissery ameonekana akishikilia msimamo wake kuwa Gavana Joho lazima kusalimisha bunduki zake zote anazomiliki kwa maafisa wa polisi na endapo atazidi kukaidi agizo hilo atatiwa mbaroni wakati wowote.
"Lazima gavana Joho kusalimisha bunduki zote anazomiliki kwa maafisa wa polisi na iwapo atazidi kukaidi tutamtia nguvuni wakati wowote , serikali iko kuhakikisha kuwa usalama wa kila Mkenya unaimarishwa", alisema Nkaissery siku ya Jumanne.
Hatua ya kupokonywa bunduki gavana Joho imejiri siku chache tu baada ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo Malindi unadaiwa kuwa viongozi wa Pwani walitumia mamlaka yao vibaya kuwashurutisha walinzi wao kuwanyanyasa wakaazi.