Martha Wangari ameitaka tume ya ardhi nchini NLC kuhakikisha inatafuta suluhu la kudumu kwa matatizo ya mashamba kwenye eneo la bonde la ufa.
Wangari akizungumza Gilgil mnamo Jumatatu alisema mizozo ya mashamba kwenye maeneo ya Naivasha na Njoro inahatarisha amani ambayo imekuwa ikishuhudiwa.
“Mambo haya yote ni yasuluhishwe na tume ya ardhi. Mohammed Swazuri anafaa ahakikishe suluhu la kudumu limepatikana,” Wangari alisema.
Seneta huyo alisema swala la mashamba huenda likaibua wasiwasi wakati ambapo taifa linaelekea uchaguzi ujao.
Kwa sasa wakaazi wa NJoro wana wasiwasi baada ya mzozo kuibuka kati ya jamii mbili kwenye eneo hilo.