Aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha TNA daktari Abdi Noor amewasuta polisi kwa kutukia nguvu zaidi dhidi ya wafuasi wa chama pinzani cha CORD.
Noor amewalaumu polisi kwa kuvuruga maandamano yaliyokuwa yameandaliwa na wafuasi wa muungano huo siku ya jumatatu.
Akiongea na wanhabari mjini Nakuru alisema kwamba maandamano hayo yalikuwa ya amani hadi pale polisi walitumia vitoa machozi kuwatawanya.
"Ni makosa kwa maafisa wa polisi kuwatawanya wakenya ambao wanatekeleza haki yao ya kikatiba . maandamano ya CORD yalikuwa ya amani hadi pale polisi walipo yavuruga na hii ni kukiuka uhuru wa kujieleza ulio ndani ya katiba" Noor alisema.
Aidha, aliitaka serikali kuheshimu uhuru wa kujieleza unaotekelezwa na wafuasi wa CORD na kuwataka maafisa wa polisi kuingia katika ofisi za IEBC wanapofanya maandamano yao ili kuondoa uvumi kwamba IEBC inalindwa na serikali.
"Uhuru wa kujieleza ni wa kila mmoja na kuna haja ya viongozi wa CORD kuruhusiwa kukutana na maafisa wa IEBC ili kuondoa hofu ya uchaguzi kuibiwa," aliongeza.