Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mkufunzi wa klabu ya Gor Mahia, Frank Nuttal, hatimaye aliruhusiwa kuondoka baada ya kuzuiliwa kwa muda na usimamizi wa hoteli moja ya kifahari mjini Nairobi.

Tukio hili lilifanyika siku ya Jumanne, kufuatia madai ya kutolipa sh239,000 ya malazi. Iliripotiwa kuwa kocha huyo alizuiliwa katika hoteli hiyo alipokuwa akijiandaa kusafiri mjini Kisumu kwa mchuano wa ligi kuu soka nchini kati ya klabu ya Gor Mahia na Chemelil Sugar. Hata hivyo, baada ya taarifa hiyo kuzagaa kwenye mtandao wa kijamii na mashabiki kuonyesha ghadhabu yao, usimamizi wa klabu ya Gor Mahia waliliingia kati suala hilo na kuyalipa madeni hayo.

Haya yanajiri wiki moja tu baada ya kocha huyo kufutwa kazi na usimamizi wa Gor Mahia na kisha kurejeshwa tena kufuatia tofauti uliozuku kuuhusu mshahara wake.

Mwezi Desemba mwaka jana, Nuttal aliliktaa pendekezo la Gor lililomtaka aupunguze mshahara wake kwa asilimia 50 kutokana changamoto za kifedha zilizokua zikiikumba klabu hiyo baada ya kukosa wafadhili.