Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Gavana wa kaunti ya Nyamira John Nyagarama amesema ifikapo juma lijalo gari la kuzima moto litakuwa limefika katika kaunti hiyo kusaidia kuzima mikasa ya moto inapotokea.

Hii ni baada ya maduka ya wafanyibiashara kadhaa katika soko la Kebirigo kuteketea usiku wa kuamkia Jumatatu huku gari la kuzima moto likikosekana kutoa msaada huo huku wafanyibiashara wakipata hasara kubwa.

Akizungumza mnamo siku ya Jumatatu mjini kebirigo wakati alipotembelea mahali ambapo mkasa wa moto ulitokea Nyagarama aliahidi kuwa gari la kuzima moto litafika katika kaunti hiyo juma lijalo.

Wakati huo huo , Nyagarama alifadhili wafanyibiashara hao waliopoteza mali yao kupitia mkasa wa moto shillingi milioni moja ili kuanzishia biashara zao upya.

“Nimesema pole kwa wale ambao walipoteza mali yao na serikali yangu imetoa millioni moja kugharamia mali yenu ili muanze biashara zenu vizuri najua hasara mliyopata ni ya uchungu,” alisema gavana John Nyagarama.

“Pia gari la kuzima moto litafika kwa kaunti yetu juma lijalo ili liwe linatoa usaidizi wa kuzima moto katika kaunti yetu,” aliongeza Nyagarama.