Share news tips with us here at Hivisasa

Gavana wa Kaunti ya Nyamira amesema kuwa vita dhidi ya ufisadi vinaweza tu kushindwa iwapo Wakenya wataungana pamoja ili kukabili ufisadi.

Akihutubia wakazi katika uwanja wa michezo wa Nyamaiya siku ya Jumamosi John Nyagarama alisema kuwa serikali yake imejitolea kupambana na ufisadi.

Nyagarama alisema serikali yake haita vumilia maafisa wafisadi na kuongeza kuwa iwapo yeyote kati ya maafisa wake atahusishwa na ufisadi, atalazimika kuwaachisha kazi mara moja.

"Ufisadi ni janga la kitaifa na kamwe hatuwezi kushida vita hivi iwapo hatutaungana pamoja kama Wakenya. Afisa yeyote atakaye husishwa na ufisadi chini ya serikali yangu anapaswa kufahamu kuwa sita sita kumuachisha kazi,” alisema Nyagarama.

Nyagarama aliwapa changamoto wakazi wa kaunti hiyo kwa kusema kuwa kila mmoja ana jukumu la kuhakikisha kuwa ufisadi umekabiliwa badala ya kulaumu uongozi wa serikali kila mara.

"Kama wananchi mna majukumu yakutekeleza hasa kwa kuripoti visa vya aina yeyote vya ufisadi kwa idara zakupambana na ufisadi,” alisema Nyagarama.