Gavana wa kaunti ya Nyamira John Nyagarama amewaomba waakazi wa kaunti hiyo kukumbatia kilimo ya kisasa ili kujiendeleza.
Kulingana na Nyagarama kilimo kina manufaa mengi ikilinaganishwa na kazi za ajira huku akiomba kila mkaazi kujihusisha kwa kilimo pamoja na biashara kujiendeleza kimaisha.
Akizungumza afisini mwake wakati akitia sahihi ya maelewano kati yake na chuo kikuu cha Jomo Kenyatta (JKUAT) na kaunti ya Nyamira katika mkataba wa kuanzisha ujenzi wa maabara ya kutengeneza miche ya ndizi katika kaunti hiyo, Nyagarama aliomba kila mkaazi kujihusisha kwa kilimo haswa ya kisasa ili kujiendeleza.
“Kilimo kina manufaa mengi kwa wakaazi ninaomba kila mmoja kujihusisha kwa kilimo biashara kujiendeleza kimaisha,” alisema Nyagarama.
Wakati huo huo, Nyagarama alisema serikali yake itajaribu kila iwezalo kushirikiana na wakulima wa kila aina kuhakikisha kilimo kimefaulu katika kaunti hiyo ili kupunguza hali ya umaskini miongoni mwa wakaazi.
“Serikali yangu itashirikiana na wakulima wa kaunti hii ili kufaulu maana kilimo hufanya vyema katika eneo letu la Kisii,” aliongeza Nyagarama.