Gavana wa kaunti ya Nyamira John Nyagarama amehimizwa kubadilisha washauri wake kisiasa ili kurejesha umaarufu wake wa hapo awali. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Haya yanajili baada ya matukio mawili ya hivi juzi ambapo gavana huyo alizomewa hadharani katika mazishi ya marehemu mheshimiwa Godfrey Masanya na lile la ziara ya rais Uhuru Kenyatta Kebirigo. 

Julius Osebe, ambaye ni mchambuzi wa siasa amemhimiza Nyagarama Kuivunja bodi yake inayomshauri kisiasa huku akiiitaja 'duni na potovu.' 

"Ushauri wangu kwa gavana Nyagarama ni aivunje na kuitupilia mbali bodi ya kumshauri kisiasa. Imekuwa duni na potovu na huenda ikamfedhehesha zaidi," alisema Osebe.

Aidha amemsihi Nyagarama kuvumbua mbinu anuwai ili kubaini na kujua chanzo cha kudhorora kwake kisiasa hivi punde.

"Nyagarama anafaa kubaini chanzo cha hali inayomkumba saa hii kisiasa. Avumbue mikakati ili kurejesha umaarufu wake wa awali," aliongezea kushauri.

Johnson Ndemo, mwanasayansi wa kisiasa aidha amemtaka Nyagarama kutafuta suluhisho la mapema kabla hali hii kuzorota zaidi ya uwezo wake kisiasa huku akiongezea kumwaarifu kuachana na washauri wake akisema huenda wana nia ya kumpotosha. 

"Mimi kama mwanasayansi wa kisiasa, namsihi Nyagarama kutafuta suluhisho la mapema kuidhibiti hali hii na vile vile aachane na washauri wake huenda wanampotosha," alisema