Gavana wa kaunti ya Nyamira John Nyagarama amejitokeza kusema kuwa serikali yake itatenga shillingi millioni 18 ili kuajiri maafisa zaidi wa ukusanyaji ushuru watakaoisaidia serikali yake kukusanya ushuru ili kuafikia malengo yake.
Akihutubia wanahabari mjini Nyamira siku ya alhamisi Nyagarama alisema ili kaunti ya Nyamira kujitoshelesha sharti kuwepo maafisa zaidi wa ukusanyaji ushuru.
"Ili kaunti hii kujistawisha kimaendeleo sharti tukusanye ushuru wakutosha na ndio maana nimetenga millioni 18 zitakazosaidia kuajiri maafisa zaidi wa ukusanyaji ushur,u kote Nyamira," alisema Nyagarama.
Nyagarama aidha aliongeza kuwa tayari serikali imetenga millioni 100, pesa zitakazoiwezesha serikali yake kuajiri vijana 50 kutoka kila eneo wodi Nyamira ili walinde chemichemi za maji, kupanda miti na pia kusafisha soko mbalimbali na hata pia kufagia barabara.
"Tuna mipango mizuri yakuhakikisha vijana wetu wetu wamepata ajira na ndio maana tumetenga millioni 100 ili kuajiri vijana 50 kutoka kila eneo la uwakilishi wodi, vijana watakaotusaidia kulinda chemichemi za maji, kufagia masoko na hata soko huku Nyamira," aliongezea Nyagarama.