Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kufuatia maandalizi ya shehere za krismasi kuendelea kupamba moto katika maeneo mengi nchini, gavana wa Kaunti ya Nyamira amewahimiza waendeshaji magari na pikipiki kuwa waangalifu.

Akihutubu kwenye mkutano wa kufunga mwaka uliohusisha idara zote za serikali ya kaunti hiyo kwenye mkahawa mmoja mjini Nyamira siku ya Jumanne, John Nyagarama alisema madereva wanastahili kuzingatia sheria za barabarani ili kulinda maisha ya wananchi hasa wale wanao safiri.

"Yafaa madereva wetu wawe waangalifu zaidi hasa msimu huu wa krismasi kwa kuwa kuna watu wengi wanao safiri kutoka sehemu moja hadi nyingine," alisema Nyagarama.

Wakati huo huo, Nyagarama aliwahimiza wakazi kutofurahia msimu wa krismasi kwa kutumia pesa nyingi bila kuzingatia mwezi wa Januari, shule zitakapofunguliwa kwa muhula wa kwanza.

"Shule zinafunguliwa upya kwa muhula wa kwanza mwezi Januari. Watu wanapaswa kuzingatia hilo ndipo wasitumie pesa nyingi kwenye msimu huu wa krismasi bila kufahamu kuwa januari inabisha hodi," alisema Nyagarama.