Gavana wa kaunti ya Nyamira John Nyagarama amejitokeza kuwarahi wakazi wa kaunti ya Nyamira hasa wakulima kukumbatia unyunyuziaji mimea maji kwa minajili ya kuongeza mazao zaidi ya shamba.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akihutubu kwenye mkutano wa kuhamazisha washikadao kuhusiana na umuhimu wa unyunyuziaji maji mashamba kwenye mkahawa mmoja mjini Nyamira siku ya Jumanne, Nyagarama alisema kuwa yafaa wakulima wakumbatie unyunyuzi maji ili kukidhi mahitaji ya kaunti. 

"Ni ombi langu hasa kwa wakulima wanaokuza mimea na mazao mbalimbali humu Nyamira kuhakikisha kwamba wananyunyuzia maji mashamba ili kuchangia katika kuongeza mazao zaidi yanayoweza kukidhi mahitaji ya wakazi wa kaunti hii," alisema Nyagarama.

Nyagarama aidha aliongeza kusema kuwa serikali yake itaendelea kuyapa masuala ya kilimo kipau mbele kwa maana kilimo ndicho kinachotegemewa pakubwa katika kuinua viwango vya uchumi nchini. 

"Sekta ya kilimo ndiyo iliyo na idadi nyingi zaidi ya wafanyakazi nchini na asilimia 80 ya wananchi wanategemea sana kilimo ili kujiendeleza kimaisha, na kwa sababu hiyo serikali yangu itaendelea kuyapa masuala ya kilimo kipau mbele kwenye mipango yake," aliongezea Nyagarama.