Gavana wa kaunti ya Nyamira John Nyagarama ameshtumu vikali hatua ya madaktari wa mifugo kudai wakulima shillingi elfu 1,500 ili kuwapa mifugo yao hasa Ng'ombe mbegu za kisasa. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Kwenye mahojiano kwa njia ya simu siku ya Jumatano, Nyagarama alisema kuwa serikali ya kaunti yake iliweka kiwango cha shillingi mia 500 kama pesa za utoaji huduma hizo.

"Ningependa kuwatahadharisha wafugaji mifugo hasa Ng'ombe dhidi ya kuwalipa madaktari wa mifugo shillingi elfu 1,500 kama pesa za utoaji huduma za mbegu kwa mifugo," alisema Nyagarama. 

Nyagarama aidha aliongeza kusema kuwa serikali yake haitosita kuwachukulia hatua kali za kisheria madaktari watakaopatikana wakikiuka agizo hilo.

"Kuna baadhi ya madaktari wa mifugo ambao labda watakiuka agizo la serikali kuhusiana na kiwango cha pesa wanachostahili kulipa wakulima ili mifugo yao ipokezwe huduma ila wacha wafahamu kwamba serikali yangu itawachukulia hatua zakisheria," aliongezea Nyagarama.