Kufuatia ongezeko la visa vya ubakaji kuendelea kuripotiwa katika maeneo mengi ya Nyamira, Gavana wa kaunti hiyo John Nyagarama amejitokeza kuwaonya vikali wale wote wanajihusisha na visa hivyo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kwenye mahojiano ya kipekee afisini mwake siku ya Jumatano Nyagarama alisema kuwa visa vya ubakaji vinaendelea kuongezeka, hali aliyosema kamwe haitovumiliwa. 

"Haiwezekani kwamba kuna wanaume wanaobaka watoto wadogo nami niketi tu na kuangalia, kwa maana nitahakikisha kwamba watu kama hao wamekabiliwa vikali kisheria," alisema Nyagarama. 

Nyagarama aidha aliwashtumu baadhi ya wazazi na walezi kwa kutoripoti visa vya ubakaji huo, hali aliyosema inachangia kuongezeka kwa visa hivyo.

"Baadhi ya wazazi wamekuwa wakificha kuripoti visa vya ubakaji, na ni himizo langu kwao kuhakikisha wanachukua jukumu la kuripoti visa hivyo na iwapo itagunduliwa kuwa wao pia huficha ukweli, basi hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao," aliongezea Nyagarama.