Kufuatia visa vya wizi wa mitihani ya kitaifa kukithiri nchini hasa katika mtihani wa mwaka jana, Gavana wa kaunti ya Nyamira John Nyagarama amejitokeza kuwaonya vikali wanafunzi dhidi ya kujihuzisha na wizi wa mitihani. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Akihutubu katika shule ya upili ya wasichana ya Sironga siku ya Jumanne, Nyagarama alisema kuwa mazoea ya wanafunzi kujihuzisha na wizi wa mitihani yanaathiri pakubwa uhalali wa matokeo. 

"Haya mazoea ya baadhi ya wanafunzi wanaoiba mitihani ya kitaifa yanaathiri uhalali wa mitihani ya kitaifa kwa maana kwa mara nyingi sisi huwasherehekea watoto wetu kuwa wamefanya vizuri kwenye mitihani ilhali si kweli," alisema Nyagarama. 

Nyagarama aidha aliongeza kwa kuwahimiza wanafunzi kutia bidii masomoni badala ya kujihuzisha na visa hivyo vya wizi wa mitihani kwa maana wazazi na walezi wa wanafunzi wengi huangaika kuhakikisha wanao wamelipiwa karo. 

"Ni himizo langu kwenu kuhakikisha kwamba mnatia bidii masomoni kwa maana wazazi wengi huangaika sana kuwatafutia karo na huu mchezo wa wizi wa mitihani sio mzuri kwa maana nikujiaribia maisha," liongezea Nyagarama.