Gavana wa kaunti ya Nyamira John Nyagarama alipata wakati mgumu kuwahutubia wakazi wa Kebirigo mapema Jumatano baada ya wakazi wa eneo hilo kumzomea hadharani mbele ya rais Uhuru Kenyatta kwenye hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kebirigo-Mosobeti.

Share news tips with us here at Hivisasa

Haya yanajiri baada ya naibu rais William Ruto kukosa kumpokeza kipasa sauti mbunge wa Borabu Ben Momanyi na badala yake kumpokeza gavana Nyagarama.

Hata hivyo ilimbidi gavana Nyagarama kusitisha hotuba yake na kupokeza kipasa sauti mbunge wa Borabu Ben Momanyi ndipo hali ikatulia.