Sasa imebainika kwamba Seneta wa Nyamira Kennedy Okongo hawanii tena kiti hicho, ha huenda akawa anamezea mate kiti cha ugavana.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Okongo amesema kuwa ameamua kutafuta kiti cha ugavana ili kuokoa wananchi wa Nyamira kutoka na 'dhuluma' za ufisadi ambazo zimekita mizizi katika kaunti hiyo.

"Mimi pamoja na ndugu zangu wengine tumeungana kuhakikisha kuwa tumeokoa Nyamira kutokana na jinamizi la ufisadi la utawala wa sasa," alisema Okongo.

Aidha, Okongo amesema ameacha kutafuta kiti cha useneta kutoka na ombi la wananchi kwamba wamemuona kutokana na utendakazi wake mwema kwa kiti cha useneta anaweza kuokoa Nyamira.

"Wananchi ndio wanatupatia kura na wakikuhitaji uwatumikie kwa sehemu yeyote unaitikia, mimi sio kiongozi ambaye anajitakia mwenyewe bali kiongozi mtumishi wa watu ambaye ako tayari kwa majukumu anayopewa na wananchi," aliongezea Okongo.

Okongo amekuwa mstari wa mbele kupigana na uongozi wa gavana wa sasa John Nyagarama, ambapo amekuwa akimkashifu gavana huyo kwa utumizi mbaya wa raslimali ya kaunti hiyo. 

Ssasa Nyagarama ana kibarua cha kuokoa kiti chake kwa upinzani mkali kutoka kwa Walter Nyambati, Erneo Nyakiba, Charles Mochama, Mwancha Okioma miongoni mwa wagombezi wengine mashuhuri.