Gavana wa Nyamira John Nyagarama amekasirishwa na jinsi gavana mwenzake wa Kisii James Ongwae amevunja mkataba walioweka wa kukusanya ushuru katika mji wa Keroka ikifahamika kuwa mji huo upo kwenye mpaka wa kaunti hizo mbili.
Akiongea na waaandishi wa habari nje ya mkahawa wa Acacia mjini Kisumu baada ya mkutano wa zaidi ya masaa matatu kati ya viongozi hao wawili, Nyagarama alisema kuwa mkutano huo haukuzaa matunda kwani walishindwa kuhafikiana kuhusu swala nzima, huku akisema kuwa Ongwae alisimama kidete kuwa mji huo wa Keroka upo kwenye kaunti ya Kisii, na kuwa maafisa wake wataendelea kukusanya ushuru bila kuhusisha wale wa kaunti ya Nyamira.
Aidha, Nyagarama amewaomba wananchi kuwa watulivu wakati serikali yake inahusisha wataalamu na viongozi wengine ili kulainisha na kutambua mipaka ya kaunti yake.
Ikiwa jambo hili litafaulu la kubaini mipaka basi kampuni ya kisii bottlers,jogoo estates, na chuo cha Gusii institute ambazo kwa hivi sasa zinalipa ushuru zao kwa kaunti ya kisii zitarejeshwa katika kaunti ya Nyamira kwani zipo katika kaunti ya Nyamira kulingana na ramani.
Hata hivyo, Gavana James Ongwae pamoja na naibu wake Joash Maangi walidinda kuzungumza na waandishi wa habari