Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Huenda wakazi wa Kaunti ya Nyamira wakapata sababu ya kutabasamu iwapo makubaliano yakujenga kituo cha huduma za wasaliano katika eneo hilo kati ya Wakfu wa Safaricom na serikali ya kaunti hiyo yatazingatiwa.

Akizungumza siku ya Jumatano baada ya kufanya kikao na meneja wa mauzo ya usimamizi wa mawimbi eneo la Magharibi mwa Kenya Mbaruk Ahmed, Gavana wa Nyamira John Nyagarama alisema kuwa kwa muda mwingi wakaazi wa kaunti hiyo hasa vijana wamekuwa wakilazimika kusafiri mbali na Nyamira ili kupokea huduma za mawasiliano hali ambayo imesababisha kutiwa sahihi kwa makubaliano hayo.

"Kwa muda mwingi wakaazi wa kaunti hii wamekuwa na matatizo ya kulazimika kuenda nje ya kaunti hii ili kupokea huduma za mawasiliano. Ni furaha kuwa hilo sasa halitakuwepo kwa maana tumeweka mikakati yakujenga kituo cha mawasiliano kwa ushirikiano na safaricom,” alisema Nyagarama.

Gavana Nyagarama alisema Wakfu wa Safaricom utaimarisha huduma za mtandao kwenye afisi za kaunti hiyo ili kurahisisha mawasiliano.

Alisema kuwa serikali yake itaruhusu kampuni ya mawasiliano ya Safaricom kufanya matangazo ya kibiashara kwa kuezeka taa kwenye barabara za kaunti hiyo, hatua itakayo imarisha mapato ya kaunti hiyo.

"Wakfu wa safaricom utaimarisha huduma za mtandao kwenye afisi zote za serikali ya kaunti hii na ni wazi kuwa huduma za mawasiliano zitarahisishwa. Tayari tumeamua kuipa kampuni ya Safaricom nafasi yakufanya matangazo yao ya kibiashiara kwa kuezeka taa za solar kwenye barabara zetu. Hiyo ni hatua mojawapo itakayo imarisha mapato ya kaunti hii,” alisema Nyagarama.