Wakaazi wa mji wa Eldoret wameonywa dhidi ya kula nyama wasiokuwa na uhakika nayo. Hii ni baada ya kupatikana kwa nyama ya mbwa iliyochinjwa hapo jana.
Nyama hiyo inasemekana ilikuwa inapaniwa kuuziwa wakaazi wasiokuwa na habari kuhusu uwezekano wa nyama kuwa ya mbwa.
Hii inajiri juma moja tu baada ya mwanaume mmoja kufikishwa kortini kwa kosa la kuuza nyama iliyokuwa bila stakabadhi kamili katoka katika Wizara ya Afya ya Umma.
Aidha visa hivyo vinakisiwa kuongezeka mjini na wakaazi wanaombwa kutoa ripoti kwa maafisa husika hasa wanaposhuku au wanapoona visa kama hivyo.
Kuingineko watu wanane walifikishwa katika mahakama ya manispaa ya Eldoret hii leo mchana kwa makosa tofautitofauti.
Watu tano kati ya waliofikishwa kortini walishtakiwa kwa kosa la kuundesha biashara ya vyakula bila ya mavazi rasmi ya kazi na kukosa barua ya afya. Washukiwa hao walitozwa faini kati ya shilingi elfu moja mia mbili na elfu mbili mia nne pesa taaslim.
Wengine wawili walipatikana kwa kosa la kulewa na kusababisha vurugu. Pia walitozwa faini ya shilingi elfu moja na mia tatu kila mmoja.
Vile vile mtu mmoja Alishtakiwa kwa kosa la kutumia maji bila leseni kutoka kampuni ya maji na alipewa kazi ya kuudumia umma kisha kuwachiliwa.
Mashtaka hayo yaliamuliiwa na Hakimu Makaazi wa eneo hilo N. N. Moseti.