Mwenyekiti wa shirika la uchapishaji vitabu la Jomo Kenyatta Foundation Walter Nyambati amewashtumu wabunge wa kaunti ya Nyamira kwa kutoshirikiana na kufanya kazi pamoja. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akihutubia wananchi mjini Nyamira siku ya Jumapili, Nyambati alisema kuwa wabunge wa Nyamira wamekuwa wakifanya siasa badala ya kushirikiana kufanya miradi ya maendeleo. 

"Wabunge wa eneo hili wamekuwa wakifanya siasa badala yakushirikiana kufanya miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao ya uwakilishi kwa kuwa sasa ni wakati wa kufanya kazi na wala sio kufanya kampeni," alisema Nyambati. 

Mbunge huyo wa zamani wa Kitutu Masaba aliongeza kumshukuru gavana Nyagarama kwa kuendelea kushirikiana na serikali kuu ili kustawisha maendeleo kwenye kaunti ya Nyamira. 

"Ninamshukru gavana Nyagarama kwa kuendelea kwake kushirikiana na serikali ya kitaifa ili kustawisha maendeleo kwenye kaunti ya Nyamira," alisema Nyambati. 

Nyambati aidha aliwarahi wakazi wa Nyamira kumwombea naibu Rais William Ruto kuhusiana na kesi ya jinai inayomkumba kwenye mahakama ya kimataifa huko Hague, Uholanzi. 

"Ninawasihi wananchi wa eneo hili kumwombea naibu Rais William Ruto kuhusiana na kesi inayomkabili ili kwamba aondolewe mashtaka ili iwe rahisi kwake kuwahudumia wakenya," alisihi Nyambati.