Familia moja katika lokesheni ya Esise kaunti ya Nyamira , Imeshikwa na butwa baada ya kesi Mbili kuwasilishwa kwa mahakama ya Keroka na wanafamilia wawili, jabo ambalo limewaacha wanakijiji wa Rusiinga katika eneo hilo vinywa wazi.
Mzozo ulizuka baada ya mmoja wa familia hiyo kuaga dunia na Ikiagunduliwa yakwamba marehemu alikuwa ameuza shamba lake lote, kwa hivyo kukakosekana pa kumzika. Mmiliki mpya Andrew Ongaga kutoka eneo la chebing’ombe, alikataa marehemu asizikwe kwenye shamba hilo kwani ni lake kwa sasa.
wakiongea na huyu mwanahabari hii leo, katika kijiji hicho cha Rusinga, mke wa marehemu Beatrice Misati alimshtaki babamkwe kwa kutomwonyesha mahala mbadala pa kumzika mpenziye kwani hakupakisha hata kipande kidogo cha shamba baada ya kuuza hekari zake Mbili.
Kwa upande mwingine Ongaga ambaye ni mmiliki amewashtaki mke wa marehemu Beatrice misati na baba ya marehemu Naftal Bosire kwa kutomrudishia pesa zake alizonunua shamba hilo kwani hao wawili wanadai aondoke kwenye shamba hilo ili kuruhusu mazishi kuendelea. Marehemu amemaliza miezi miwili katika chumba cha kuifadhi maiti cha Keroka.
Chifu wa lokesheni hiyo Alfred Onchong’a amethibitisha hayo na kusema mke wa marehemu hana makosa kwa kuagiza babamkwe kumwonyesha mahala pengine pa kumzika mumewe kwa kuwa ni wa familia hiyo.
Beatrice Misati, ambaye ni mke wa marehemu amekataa kuwasilisha stakabadhi za shamba hilo na vitambulisho huku Ongaga ambaye ni mmiliki akisema alinunua shamba hilo millioni moja na yuko tayari kurudishiwa pesa zake na kuondoka.
Mke wa marehemu amesema hatatoa pesa zilizo kwa benki na kuagiza wanafamilia kufanya mchango na kurudishia mnunuzi pesa zake. Jambo ambalo limewakasirisha wanafamiliana kuwashangaza wanakijiji.
Kufikia sasa wanafamilia hao wanasubiri mahakama ya Keroka kutoa tarehe rasmi ya kusikizwa kwa kesi hizo.