Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mbunge wa eneo bunge la Mugirango Kusini Manson Nyamweya ameahidi kukarabati barabara za eneo bunge hilo ili kuimarisha sekta ya uchukuzi kwa wakulima na wafanyibiashara wa eneo hilo.

Hii ni baada ya wakazi hao kuomba kukarabatiwa barabara za eneo hilo kwa muda mrefu.

Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatano mjini Kisii, Nyamweya aliahidi kuzikarabati barabara za eneo bunge lake kwanzia mwaka ujao ili kutimiza ahadi alizotoa kwa wakaazi.

Kulingana na mbunge huyo, baadhi ya barabara ambazo zitakarabatiwa ni barabara za Etago-Nyamwaya, Nyangweta–Kiagware na Mochengo-Nyamaiya.

Nyamweya aliahidi kufanya maendeleo mengi ili kutimiza ahadi alizotoa kwa wakaazi kabla ya mwaka mwaka wa 2017 kutimia.

“Mimi kama mbunge wa Mugirango Kusini nilichaguliwa na wakaazi wa eneo hili ili nilete maendeleo. Nitajaribu niyafanye yale yote niliahidi kufanya,” alisema Nyamweya.

Aliongeza, “Kufikia sasa, nimeyafanya mengi lakini sijaridhika kwani bado sijakifikia kiwango kinachofaa.”

Nyamweya aliahidi kushinikiza serikali ya Kaunti ya Kisii kuweka miradi ya maji katika eneo bunge lake ili wakaazi wasiwe wanasumbuka kwa kutembea masafa marefu wakitafuta maji.