Msanii Nyota Ndogo katika hafla ya awali. Picha/ nairobinews.nation.co.ke

Share news tips with us here at Hivisasa

Nyota Ndogo, msanii kutoka Mombasa, ameitaka serikali kuunda sheria itakayoangazia maswala ya mavazi, hasaa miongoni mwa wanawake.

Haya yanajiri baada ya Nyota Ndogo kumwona mwanamke aliyekuwa amevalia vazi ambalo halikuwa limemsitiri vizuri.Msanii huyo aliweka picha ya mwanamke huyo katika mtandao wake wa Facebook, na kutoa wito huo kwa serikali katika ujumbe alioubatanisha na picha hiyo."Kama Kenya tunaserikali tafadhali serikali watoto wetu huku ndio wamefikia. Hii ilikua Mombasa jana (Jumanne). Hizi sio kiki tena niudhalilishaji wa hali ya juu. Serikali tafadhali wanawake mulio bungeni hili swala linawahusu. Inabidi muweke vipimo vya mavazi........Wallai jamani hii ni nini? tumefika hapa?" aliandika Nyota Ndogo.Mwanamke huyo alikuwa amevalia vazi jekundu kuashiria sherehe ya siku ya wapendanao iliyoadhimishwa siku ya Jumanne kote ulimwenguni.Vazi hilo lilikuwa wazi likionesha asilimia kubwa ya mwili wake, ikiwemo sehemu nyeti.Shutuma hizo zilipokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa Nyota Ndogo huku baadhi yao wakiunga mkono mavazi ya mwanamke huyo aliyekuwa katika klabu moja huko Mombasa.