OCPD wa eneo la Changamwe, Stephen Chateka, ameaga dunia.
Chateka anaripotiwa kufariki alipofikishwa katika hospitali moja ya kibinafsi mjini Mombasa siku ya Jumamosi.
Akidhibitisha ripoti hizo, Kamanda wa polisi Kaunti ya Mombasa Peterson Maelo alisema marehemu aliaga dunia mwendo wa saa sita mchana baada ya kupelekwa hospitalini.
Maelo alisema Chateka alikuwa akiugua ugonjwa wa kisukari na presha, na alizidiwa ghafla akiwa ofisini mwake.
Mapema mwaka huu, idara ya polisi ilipoteza kamanda wa polisi wa Migori Moses Chepyegon, katika kisa sawa na hicho.
Chepyegon alifarika muda mfupi baada ya kufikishwa katika hospitali ya Migori Level Four.