Mahakama ya Mombasa imeagiza OCS wa Kituo cha polisi cha Bandari kufika kortini kuhusu kesi ya ulaghai dhidi ya maafisa wa polisi.
Mahakama imemtaka OCS huyo kueleza sababu ya afisa wa upelelezi wa kesi hiyo ya ulaghai kutofika kortini.
Washukiwa hao, Ali Yusuf na Nahim Hussein, wanadaiwa kupokea gari kupitia njia ya ulaghai kutoka kwa Shahzid Yusuf.
Hapo awali, mahakama iliambiwa kuwa washukiwa hao walitekeleza kitendo hicho katika Kaunti ya Mombasa.
Hakimu wa Mahakama ya Mombasa Henry Nyakweba ameahirisha kesi hiyo hadi afisa mpelelezi wa kesi hiyo atakapofika mahakamani.