Kinara wa Nasa.Raila Odinga. Ametakiwa kuzingatia Katiba katika kuwa Rais wa nchi ya Kenya. [nairobinews.nation.co.ke]Baraza la Wazee Kaunti ya Mombasa wamemtaka kinara wa upinzani Raila Odinga kuzingatia katiba na kubatilisha azma yake ya kutaka kuapishwa.Mwenyekiti wa baraza hilo jijini Mombasa, Mohammed Jahazi amesema NASA inastahili kuiheshimu katiba ambayo hairuhusu uongozi wa Rais zaidi ya mmoja.“Nasa inafaa kuheshimu na kufuata katiba,katiba haikubali nchi kuwa na maraisi wawili,” alisema Jahazi.Akizungumza siku ya Alhamisi, aliwataka vigogo wa Nasa kufanya majadiliano na serikali ya Jubelee kwa manufaa ya wakenya wote badala ya kuzozana kisiasa.“Majadiliano ndio njia pekee ya kumaliza mzozo huo wa uongozi kati ya Jubilee na Nasa,waache kugombana,waje pamoja waelewane,” alisema Jahazi.Jahazi alisema muda mwingi ulipotezwa msimu wa siasa hivyo wakati umefika kwa viongozi kutambua wajibu wao wa kuwahudumia wananchi kwa kutekeleza miradi itakayowanufaisha.“Muda mwingi ulipotezwa wakati wa siasa,sasa tutumie muda huu wa sasa kuimarisha na kuboresha maendeleo nchini”,alisema Jahazi.Kauli ya Jahazi inajiri siku chache baada ya Muungano huo kuahirisha shughuli ya kumwapisha Raila iliyoratibiwa kufanyika hapo jana na kusema kuwa utatoa tarehe ya kutekelaza shughuli hiyo baadaye.
MOMBASA
Odinga atakiwa kujadiliana na Uhuru kuhusu uongozi
ADVERTISEMENT
Share news tips with us here at Hivisasa
Thank you for reading my article! You have contributed to my success as a writer. The articles you choose to read on Hivisasa help shape the content we offer.
-Osman Suleiman