Seneta wa kaunti ya Nyamira Kennedy Okongo amewashutimu walimu wakuu wanao ongeza karo ya shule kiholela holela, na kuwataja walimu hao kama wafyonza wazazi maskini bila huruma.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

"Walimu hawa ambao huongeza karo zaidi kutoka kile kiwango cha serikali imeweka in walaghai na wafyonza, wanawezaje ongeza karo kutoka kile kiwango kimewekwa hadi kiwango chao," aliuliza Okongo.

Serikali iliweka kiwango cha karo kiwe elfu hamsini kwa shule za kitaifa, lakini shule zingine zimekiuka sheria hiyo.

Okong'o alitaja mwalimu mkuu wa shule ya wasichana ya Sironga kuwa mmoja wa walimu walaghai huku akiahidi kutaja majina ya walimu wengine.

Seneta huyo vile vile alisema kwamba atalipeleka swali hilo la wazazi kuongezewa karo katika serikali kuu na kulikabidhi waziri wa elimu Fred Matiangi na kuwaomba wazazi wasilipe karo yoyote zaidi kuliko ile ya serkali.

Seneta alikuwa alizungumza haya siku ya Jumamosi katika kanisa moja wadi ya Bomwagamo katika kaunti ya Nyamira.