Mwenyekiti wa chama cha ODM tawi la Nakuru Peter ole Osono amefutuilia mbali madai ya kuwepo kwa mvutano baina ya wanachama wa chama hicho katika kaunti hiyo licha ya kushuhudiwa kwa vita miongoni mwa wanachama siku ya Jumamosi katika afisi za chama hicho jijini Nakuru.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Vita vilizuka katika hafla iliyoandaliwa kusheherekea ushindi wa viongozi wapya wa chama hicho waliochaguliwa mwezi Oktoba mwaka uliopita na kusitisha shughuli hiyo kwa zaidi ya saa moja unusu huku Sam Muche anayedaiwa kuongoza mrengo unaopinga uongozi uliochaguliwa akishambuliwa baada ya kujitokeza katika sherehe hiyo bila kualikwa.

Ole Osono hata hivyo akihutubia wanahabari ameelezea kuwa wananchama wako imara kutumikia wafuasi wao na kuwa rabsha hizo hazina sababu yoyote ya kuwatenganisha.

"Sisi katika chama cha ODM huku Nakuru hatuna mvuragano wowote, tuko pamoja kama wanachama kuendelea na shughuli yetu ya kutumikia chama pamoja na wananchi kwa ujumla. Lengo letu ni kuhakikisha chama chetu kinapata umaarufu zaidi katika eneo hili ambalo ni ngome ya Jubilee kabla ya uchaguzi wa mwaka ujao" Ole Osono alisema.

Muche ni mmojawapo watu ambao wanapinga kuchaguliwa kwa viongozi wa chama hicho katika eneo hilo lakini Ole Osono amewakashifu wanaoegemea upande huo na kuwaomba waungane pamoja katika kumpa kiongozi wao Raila Odinga umaarufu zaidi.

"Ni jambo la kusikitisha kuona watu ambao si wanachama wetu wakijitokeza na kuzua randha katika mikutano yetu wakiwa walevi. Tayari tumezungumz na wanachama na tuanakemea zaidi jambo hili. Huu ni wakati ambao tunaomba kila mmoja aje aungane nasi katika kuimarisha chama hiki badala ya kuleta mvurugano na kueneza maneno yasiyofaa, huo ni kupoteza wakati bure," Ole Osono aliongeza.