Katibu mkuu wa chama cha TNA Onyango Oloo ameushtumu mrengo pinzani wa Cord kufuatia mihemko iliyoshuhudiwa siku ya Alhamisi katika bunge la taifa, na kusema kuwa kisa hicho kinafaa kuchukuliwa hatua kali.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Katika kikao na wanahabari jijini Kisumu, Oloo amesema mtafaruku huo ulisababishwa na baadhi ya wanachama wa ODM waliokuwa na lengo mbaya kuhusiana na mswada huo, na walikuwa wamejiandaa kuvuruga zoezi hilo.

Oloo amesema ingekuwa vyema iwapo mrengo pinzani ungeruhusu kujadiliwa kwa mswada huo, na wala sio kuvuruga zoezi lote bungeni.

Aidha, amesema mswada huo ambao rais ameutia sahihi kuwa sheria ni bora, na utasaidia katika kukabiliana na visa vya utovu wa usalama nchini.

“tumeon vile ambavyo wamefanya katika uchaguzi wao wa chama, na visa hivyo ndio walipeleka bungeni ili kuleta vurugu isiyostahili,” alisema Oloo.

Oloo amempongeza rais kwa kutia sahihi kwa mswaada huo, akisema utasaidia sana kutuliza visa vya ugaidi ambavyo vimekidhiri katika siku za hivi majuzi.