Seneta wa Kaunti ya Mombasa Hassan Omar ametoa wito kwa viongozi wa kaunti ya Mombasa na idara ya usalama katika Kaunti hiyo kusuluhisha mizozo iliyoko kati yao ili kuangazia maswala mengine ya maendeleo.
Akizungumza na wanahabari mjini Mombasa siku ya Jumatatu, seneta huyo alisema kuwa mzozano baina ya viongozi hao ni ishara kuwa wameupoteza mwongozo wa mambo muhimu ambayo yanafaa kuangaziwa.
Wakati huo huo, seneta huyo pia alisema kuwa katiba mpya imebainisha majukumu ya gavana na yale ya kamishna wa kaunti na kwa kufanya hivyo, hakufai kuwa na mizozano yoyote baina ya viongozi hao kwa kuwa kila mmoja ana majukumu yake.