Seneta wa Kaunti ya Mombasa Hassan Omar ameitaka serikali kuu kuingilia kati ili kuvikomesha visa vya Wakenya kudhulumiwa katika mataifa ya mashariki ya kati.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Omar amewataka viongozi wenzake nchini kutolinyamazia suala hilo, kwa kusema Wakenya wanaohangaishwa katika nchi hizo ni wengi.

Akiongea mjini Mombasa siku ya Ijumaa, baada ya suala ya jioni, Omar alisema ni jambo la kusikitisha kuona serikali ikikosa kuchukua hatua licha ya visa hivyo kuripotiwa mara kwa mara.

“Tunasikitika kuona kuwa Wakenya wanateswa katika mataifa ya Uarabuni na serikali bado haijaingilia kati swala hilo. Sisi tunakashifu visa hivyo vikali na tutahakikisha tunafanya kila juhudi kuwaokoa Wakenya wenzetu wanaopitia mateso katika mataifa hayo,” alisema Omar.

Haya yanajiri huku Wakenya wakikisiwa kupitia mateso zaidi katika nchi za Uarabuni, ambako idadi kubwa ya Wakenya husafiri kusaka ajira