Serikali ya kaunti ya Mombasa imetakiwa kubadilisha mpango wa ujenzi wa nyumba za serikali zinazotazamiwa kujengwa karibuni.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza na wanahabari afisini mwake, siku ya Jumanne, seneta wa Mombasa , Hassan Omar ameitaka serikali ya kaunti kuwashauri wakazi wanaishi katika nyumba hizo kabla ya ujenzi kuanza.

Omar ameiaka hatua hiyo kuwa mbinu ya kuuzwa kwa nyumba hizo na kuongeza kuwa raslimali za kaunti zimenyakuliwa na mabwenyenye wanaojinufaisha kibinafsi.

Amewasisitiza wakazi hadi pale sheria zinazofaa zitakapo fuatiliwa kikatiba.

Mradi wa ujenzi wa nyumba mpya za serikali ya kaunti ya Mombasa unatarajiwa kugharimu takribani shilingi bilioni mia mbili.