Uhasama baina ya Gavana wa Kaunti ya Mombasa Hassan Joho na Seneta Hassan Omar huenda ukachukua mkondo mwingine baada ya seneta huyo kukosa kuhudhuria hafla ya uzinduzi rasmi wa ruwaza ya 2035 ya kaunti hiyo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Hafla hiyo iliyoandaliwa siku ya Jumamosi katika uwanja wa mchezo ilihudhuriwa na viongozi kadhaa wakiwemo Gavana wa Kaunti ya Lamu Issa Timmamy, mbunge wa Mvita Abduswamad Nassir, Mbunge wa Kisauni Rashid Bedzimba na mbunge wa Jomvu Twalib Badi, miongoni mwa viongozi wengine.

Inadaiwa kuwa hatua ya Seneta Omar kukosa kuhudhuria hafla hiyo ilichangiwa pakubwa na msimamo wake kuwa atawania kiti cha ugavana wa kaunti hiyo katika uchaguzi mkuu ujao.

Itakumbukwa kuwa Omar amekuwa katika mstari wa mbele kuikosoa serikali ya Joho, kwa kudai kuwa gavana huyo hajatekeleza maendeleo yoyote kwa wakaazi wa Mombasa.