Seneta wa Mombasa Hassan Omar amesema Chama cha Wiper hakitakubali mchujo wa mapoja katika muungano wa Cord.
Sarai ambaye ni katibu mkuu wa chama cha Wiper, ameeleza kwamba mchujo wa pamoja ndani ya Cord ni sawa na kupoteza mwelekeo wa vyama vya kisiasa.
“Hatua ya kuwa na mchujo wa pamoja ni sawa na kuvunja vyama vya muungano wa Cord,” alisema Omar.
Seneta huyo alisema kuwa chama cha Wiper kitatangaza mwelekeo wake rasmi siku ya Jumamaosi kuhusu uhusiano wao na muungano wa Cord.
“Tutatangaza msimamo wetu wa chama Jumamosi ijayo,” alisema Omar.
Aidha, Omar alisema kuwa sharti mgombea wa rais katika muungano wa Cord kutangazwa mapema ili apigiwe debe kwa wakati ufaao.
“Mgombea rais wa muungano wa Cord anafaa kutangazwa mapema ili apigiwe debe mapema,” alisema Omar.
Tayari chama cha ODM kimemteua Raila Odinga kama mgombea wake wa urais.
Chama cha Wiper kinaendeleza kampeni zake katika eneo la Pwani baada ya ODM kufanya kampeni zake juma lilopita.