Seneta wa kaunti ya Mombasa Hassan Omar amepongeza uamuzi wa mahakama ya ICC dhidi ya kesi ya Naibu Rais William Ruto na Mwanahabari Joshua Sang, akisema kuwa kutupiliwa mbali kwa kesi hiyo huenda kukupunguza joto la kisiasa na uhasama uliyopo baina ya viongozi wa tabaka fulani.
Akiongea na wanahabari mjini Mombasa siku ya Jumatano, Sarai alisema kuwa kuamuliwa kwa kesi ya Ruto kulichukua hekima na uamuzi wa busara ambao umesaidia pakubwa wakenya kwani joto la kisiasa na uhasama wa kikabila utasitishwa.
Omar alisema kuwa kuendelezwa kwa kesi hiyo kungesababisha uhasama wa kikabili haswa ikizingatiwa kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2017 unakaribia na tayari mchakato wa kisiasa na joto la kisiasa limeanza kupamba moto nchini.
Kiongozi huyo aliitaka serikali kutumia taasisi za humu nchini pamoja na mahakama kuhakikisha kuwa waathiriwa wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007 /2008 wanalipwa fidia.
"Mahakama ya ICC ilitoa uamuzi wa busara na tuna imani kuwa serikali italiangazia swala la waathiriwa wa ghasia na kuwalipa fidia sambamba na kuwa haki zao, na tumani la kuwepo na amani pia lipo kwani uamuzi huo umeondoa lile joto la kisiasa," alisema Omar.
Seneta wa kaunti ya Mombasa Hassan Omar akizungumza na wanahabari kuhusu uamuzi wa ICC dhidi ya kesi ya Ruto. Amepongeza uamuzi huo kwa kina.